Bethidei Ya Wolper Yatikisa Jiji la Dar (Pichaz + Video)

Muigizaji Jackline Wolper akisaidiwa kukata keki katika Ukumbi wa Bucket, Masaki, Dar, usiku wa kuamkia leo ambako mastaa mbalimbali waliungana naye na kumwagia zawadi mbalimbali.

Wolper akimlisha keki Barnaba Classic (wa pili kushoto).

…Akimlisha keki Moze Iyobo huku Anti Ezekiel (kushoto) akishuhudia.

…Akimkaribisha Barnaba kupiga burudani.

…Akicheza kwa hisia wimbo wa Barnaba aliye jukwaani akitumbuiza.

Msanii Amber Lulu (kulia) akishindana kukata mauno na Wolper.


UKUMBI wa Buckets, uliopo Masaki jijini Dar, jana usiku ulilipuka kwa shamra kibao pale muigizaji Jackline Wolper alipokuwa akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa pamoja na mashabiki wake.

 

Katika sherehe hiyo, mbali na muigizaji huyo kuzindua ‘app’ yake ambayo atakuwa akiweka kazi zake zote za sanaa  na biashara zake, alisindikizwa na mastaa wengi wakiwemo Steve Nyerere, Giggy Money, Amber Lulu.

 

Mastaa wengine waliofurika kwenye sherehe hiyo ni pamoja na Tunda, Petty Man, Country Boy, O.M.G, PCK, Anty Ezekiel, Barnaba, Moses Iyobo, Mon Central Zone, Husna Maulid, Duma na wengine wengi.

 

Akizungumzia sikukuu hiyo, Wolper alisema: “Asanteni kwa wote mliokuja kunipa sapoti kwenye siku yangu ya kuzaliwa. Kimsingi nilizaliwa siku ya jana (Jumatano), tarehe 6 ya mwezi huu ambapo nilisherehekea siku hiyo na watoto yatima.

 

“Lakini leo tarehe saba nimeamua kusherehekea pamoja na nyie mashabiki zangu. Naombeni muendelee kuniunga mkono pia kwenye App yangu ambayo nimeizindua leo.”

(HABARI MWANDISHI WETU | GLOBAL PUBLISHERS)


Loading...

Toa comment