The House of Favourite Newspapers

BETIKA GUMZO KARIAKOO

GAZETI la Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya GlobalPublishers na kutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, limeendelea kuwa gumzo kila kona ya Tanzania.

 

Betika ambalo linaingia mtaani kila Jumatano lina kurasa 20 za rangi, makala na odds za kampuni mbalimbali, pamoja na takwimu za ligi tofauti duniani.

Kila linapoingia mtaani, maofisa masoko wa Global Publishers hutembelea mitaa mbalimbali na leo Jumatano, maofisa masoko hao walitembelea mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

 

Wasomaji kadhaa waliokutwa na maofisa masoko hao, walionekana wakilizungumzia vizuri gazeti hilo hali iliyozua gumzo.

Tangu gazeti hilo liingie mtaani, hivi sasa ni wiki ya 23 na bado limeendelea kuwa gumzo kila kukicha.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo.

Mgema aliongeza kuwa, bei yao ya matangazo ni nafuu hali inayowavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kujitangaza na gazeti hilo.

 

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wotenchini.

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba
0755826488 na 0712595636 au barua pepe
[email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza
kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group.

 

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa
biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram,
Facebook, Twitter na Global TV Online,” alisema.

Comments are closed.