Betika Laendelea Kugombewa Tabata

MAPEMA leo Jumatano, Machi 26, mwaka huu timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Tabata Mawenzi jijini  Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi zaidi gazeti hilo ambalo limekuwa kimbilio kwa wadau wa kubeti.
Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wazee wa kubeti wameendelea kulisifia kwa ujio wake huo kutokana na linavyoendelea kuwanufaisha katika kujipatia mkwanja kutokana na miongozo mizuri iliyopo ndani ya gazeti hilo.
Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.
Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.
Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.
Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.
Toa comment