The House of Favourite Newspapers

Betika Laendelea Kunufaisha Wafanyabiashara Kariakoo

0
MAPEMA leo Jumatano, Januari 14, mwaka huu (2020) timu ya maofisa masoko ya Global Publishers imetembelea maeneo ya Temeke-Mwembeyanga, Kariakoo na maeneo mengine jijini  Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi zaidi gazeti la Betika.
Katika mchakato huo, wafanyabiashara wameelezea furaha yao hususani masuala ya kubeti na kuwapa fursa ya kutangaza nalo.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya ‘betting’ na ‘lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha masuala ya michezo ya kubeti.
Heshima ya Betika imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia kwak tena kwa bei nafuu.

Watu wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

NA DENIS MTIMA | GPL
Leave A Reply