The House of Favourite Newspapers

Betika Lafungua Mwaka Mpya 2020 Buguruni

0
MAPEMA leo Jumatano, Januari Mosi, 2020 (siku ya mwaka mpya) timu ya maofisa masoko ya Global Publishers imetembelea maeneo ya Buguruni  jijini  Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi za Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wazee wa kubeti wamesema kuwa huku wakisherehekea kuuona mwaka mpya wanaenda sambamba na kusoma Gazeti hilo.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Na Denis Mtima | GPL
Leave A Reply