The House of Favourite Newspapers

BETIKA LAINGIA MTAANI KIBABE, WADAU WALIPONGEZA

 

GAZETI namba moja na la kijanja linalohusu ishu nzima za kubeti lijulikanalo kwa jina la BETIKA ambalo linatolewa bure, leo Jumatano, Februari 13, 2019 limeingia mtaani rasmi kwa mara ya kwanza na litakuwa mtaani kila Jumatano.

 

 

Mapema leo, timu nzima ya maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, imetinga mtaani kwa ajili ya kulinadi gazeti hilo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam vikiwemo vitongoji vya Mwenge, Sayansi na Morocco.

 

 

Akizungumzia juu ya ujio wa gazeti hilo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema  kampuni hiyo imeamua kuliingiza gazeti hilo mtaani kwa lengo la kukidhi haja za wafuatiliaji wa soka na wanaojihusisha na masuala ya kubeti.

 

 

“Gazeti hili ni mahsusi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti. Litakuwa linatoka bure,” alisema Mgema.

 

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

 

 

Baada ya kuingia mtaani leo, watu wanaojihusisha na masuala ya kubeti wamelipongeza gazeti hilo kwa kusema kuwa litakuwa mkombozi wao katika ishu zao hizo kwani litawarahisishia kujua kila kampuni na odds zake pamoja na kufahamu njia rahisi za kubeti na kushinda.

 

Gazeti hilo pekee nchini ambalo linakuhabarisha kuhusiana na michezo na burudani, limekuwa kivutio cha wahusika mbalimbali wanaoshiriki michezo ya kubashiri matokeo na ile ya bahati nasibu.

 

 

Akizungumzia ujio wa gazeti hilo, Kezilahabi Peresi,  ambaye ni Ofisa Masoko wa Gazeti la Betika, alisema ndani ya gazeti hilo wasomaji watapata makala kali za burudani na michezo bila kusahau hadithi kali ya kusisimua.

 

 

“Zaidi ya habari na uchambuzi wa mechi mbalimbali za ligi za nje, gazeti hili litakuwa linakuletea matangazo mbalimbali kutoka katika kampuni zinazoendesha michezo ya kubahatisha. Ndani ya Betika, utapata taarifa zote kuhusu kubeti na mbinu utakazoweza kutumia kubeti na kushinda.

“Wachambuzi wetu wa ndani na nje ya nchi tulionao watakusaidia kupata mwelekeo mzuri wa mechi zitakazochezwa katika wiki husika ili kukusaidia kufanya uchaguzi mzuri wa timu utakazobeti. Sisi Betika tunaamini, gazeti letu ni fursa nzuri kwa wabetiji wote kuelewa kwa undani kuhusiana na michezo ya kubahatisha, mambo ya kuzingatia ili kubeti kwa mafanikio na kuvuna pesa kwa wingi.

 

 

“Mbali na habari na uchambuzi wa michezo na burudani, tutakuletea taarifa za watu waliotajirika duniani kupitia michezo ya kubahatisha,” alisema Peresi na kuongeza:

 

“Aidha, tumetenga sehemu maalumu kwa ajili ya kuweka mikeka ya kubeti kutoka katika kampuni mbalimbali. Ni imani yetu Betika litakusaidia kuwa mbetiji wa faida badala ya kuwa msindikizaji. Sisi Betika ni tofauti na magazeti mengine, gazeti letu haliuzwi; utalipata bure kabisa. Kwa msingi huo, ukikutana na gazeti hili mahali popote, usikubali kutoa fedha yako, utatakiwa kuchukua bure.

 

 

“Timu nzima ya Betika tuna wahakikishia tumejipanga vilivyo kukuhabarisha na kukupa mbinu za kuwa mbetiji bora, lakini milango ipo wazi kutoa maoni yako kwa lengo la kuboresha zaidi. Hatutasita kupokea maoni na kuyafanyia kazi, yale yaliyo bora na yenye tija. Jione sehemu ya Betika kwa kututumia maoni yako kupitia mawasiliano yetu yaliyomo ndani ya gazeti hilo.

“Karibuni sana Betika, kupata maujuzi ya kuvuna mahela.”

Kwa yeyote ambaye anatangaza na Gazeti la BETIKA pia atapata ofa ya kutangazwa bure katika mitandao mbalimbali ya kijamii na tovuti pamoja na channel za online.

 

Mteja atapata ofa ya biashara yake kutangazwa katika channel ya YouTube ya Global TV Online, tovuti ya Global Publishers na kurasa zake zote za mitandao ya kijamii ya Global. Karibu sana!

Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kwa namba 0659 472001 au 0659 190090 au barua pepe: [email protected]

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.