The House of Favourite Newspapers

BETIKA LANOGESHA RAHA YA WANAMSIMBAZI TAIFA

 

Shabiki wa Simba akichekelea zawadi ya tiketi ya kumuona mnyama akimchinja AS Vita akiwa na gazeti la Betika

LIKIWA limetimiza mwezi mmoja tangu liingie mtaani, Gazeti la Betika limezidi kutikisa ambapo kila siku wasomaji wamekuwa wakilimwagia sifa kemkem.

 

Gazeti hilo hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huwa linatoka kila Jumatano.

Mashabiki wa Simba wakipata uhondo wa gazeti la bure la Betika kabla ya kuingia uwanjani kuona namna mnyama alivyotinga robo fainali Ligi ya Mabingwa

Kila likitoka, maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, huingia mtaani kupata maoni ya wasomaji ambapo wengi wameonekana kulimwagia sifa.

 

Jana Jumatano, maofisa masoko hao walitinga maeneo ya Msimbazi Center, Ilala hadi Buguruni na kuzungumza na watu kadhaa juu ya gazeti hilo ambalo linahusu zaidi masuala ya kubeti.

Mashabiki wa Simba wakisoma gazeti la Betika jana Uwanja wa Taifa

“Gazeti hili ni zuri, ukilisoma hata kama hauna mpango wa kubeti basi lazima ubeti kwa sababu linakupa njia nzuri ya kushinda na mara kadhaa watu wanashinda kutokana na mbinu zilizopo humu ndani,” alisema mmoja wa wasomaji.

Mashabiki wa Simba wakichekelea kupata nakala ya gazeti la Betika jana Uwanja wa Taifa

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokea ya gazeti hilo kila siku yanazidi kuwa juu hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.

 

“Gazeti hili ni mahususi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti.

Gazeti la Betika likiwa mikononi mwa mashabiki wa Simba baada ya kupata nakala yao bure jana

“Tangu liingie mtaani, tumepata mrejesho mzuri kwamba wasomaji wanalihitaji sana, hivyo tutaendelea kuwapa vitu vizuri wasomaji wetu ili kukata kiu yao.

 

“Lakini ukingalia toleo la leo (jana), lina mambo mengi yanayohusu michezo ya kimataifa kama mechi ya Man U na PSG, hivyo watu wa kubeti wanapata maujanja ya kubashiri mchezo huo na kushinda,” alisema Mgema.

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

MASHABIKI wa Simba wakiwa makini kupitia data za gazeti la bure la Betika jana.

Z

Comments are closed.