BETIKA LAWAVUTA KWA KASI WASOMAJI

WASOMAJI wa Gazeti la Betika maeneo ya Kariakoo na Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, wamesema kwamba gazeti hilo kila siku linazidi kuwapa ulaji.

Ulaji ambao wanaupata wasomaji hao ni kushinda kirahisi wanapobeti mechi mbalimbali za soka zinazochezwa duniani, hasa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri.

“Hivi sasa utaona kuna michuano ya Afcon, Betika ambalo ni gazeti linalojihusisha na masuala ya kubeti, linatupa mwanga mzuri wa kushinda tunapobeti.

“Gazeti hili linatupa ulaji kwani kabla ya hapo tulikuwa tunabeti lakini kushinda inakuwa ngumu, hivi sasa ukisoma Betika kuna maujanja fulani ya kubeti unayapata na kurahisisha kazi yako ya kubeti,” alisema mmoja wa wasomaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Issa.

Ikumbukwe kuwa, Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

Kila linapoingia mtaani, maofisa masoko wa Global Publishers hutembelea mitaa mbalimbali na jana Jumatano walitembelea Kariakoo na Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema amesema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

“Wanaohitaji kutangaa nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe betika255@gmail.com, bei zetu ni nafuu, mhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group.

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online,” alisema.


Loading...

Toa comment