The House of Favourite Newspapers

Bi Chau; Bado anasumbuliwa na mapedeshee

0

biChauKARIBU tena msomaji katika kolamu hii inayokuunganisha na mastaa mbalimbali wa muziki, utangazaji na filamu hapa nchini na kupata fursa ya kuwauliza maswali ambayo yamekuwa yakiumiza kichwa huyapatii majibu. Leo tunaye mkongwe katika filamu na Mtangazaji, Chausiku Salum ‘Bi Chau.’

Msomaji: Wewe ni staa japo umri umeenda, wanaume wengi wenye fedha ‘pedeshee’ wanapenda kutoka na watu maarufu, husumbuliwi na watu hao?

Bi Chau: Nasumbuliwa sana lakini najitahidi kukabiliana na changamoto hiyo sababu ndiyo ustaa tena.

Msomaji: Unazungumziaje tasnia ya filamu kutawaliwa na skendo ya ufuska kuliko kazi?

Bi Chau: Ni kweli sikatai kuna ufuska mwingi katika tasnia hii ya filamu mpaka imefikia hatua wasanii wanabadilishana wanaume japo si wote ila wanapaswa kujiheshimu.

Msomaji: Nasikia una dawa za kurudisha usichana kwa mwanamke, ni kweli?

Bi Chau: Si kweli, sina dawa za kurudisha usichana kwa mwanamke na sijawahi kufanya hivyo.

Msomaji: Wasanii gani unawakubali nchini?

Bi Chau: Kwenye muziki namkubali sana Lady Jaydee na upande wa filamu ni mimi mwenyewe.

Msomaji: Kusuta umefundishwa au ndiyo asili yako, je, una miaka mingapi kwa sasa?

Bi Chau: Kwanza nianze na la kuzaliwa, nimezaliwa Kariakoo na kwenye umri ni siri yangu. Kuongea ni kipaji changu na ndicho kinachoniingizia kipato hivi sasa.

Msomaji: Una watoto wangapi na umedumu kwenye ndoa kwa muda gani?

Bi Chau: Nilikuwa na watoto wawili wa kike ila mmoja amefariki, nipo kwenye ndoa tangu mwaka 1985.

Msomaji: Wewe na marehemu Mzee Small mlikuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi?

Bi Chau: Hapana! Mzee Small alikuwa kama bosi wangu kwenye kazi za filamu na tulikuwa tukiheshimiana sana.

Msomaji: Bi Chau nimekuwa nikikufuatilia kazi zako kwa muda mrefu lakini sijajua wewe ni mwenyeji wa wapi?

Bi Chau: Asante sana, mimi ni mwenyeji wa Tunduru katika kijiji kimoja kinaitwa Masakacha.

 Msomaji: Mbona upo kimya kwenye uigizaji?

Bi Chau: Nimeacha sanaa muda kidogo, kwa sasa nimejikita zaidi kwenye utangazaji, kutokana na utangazaji huo nimeweza kujenga nyumba kubwa tu.

Leave A Reply