The House of Favourite Newspapers

Bi Hindu Alivyomkacha Mzee Kilomoni na Kutimkia kwa Mo Dewji

0
Bi Hindu.

MUDA mfupi baada ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko juu ya uendeshaji wa timu hiyo na kumpatia nafasi mfanyabiashara bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’, mwanachama wa timu hiyo, Chuma Suleiman ‘Bi Hindu’ ameibuka na kufunguka kuwa anaungana na wanachama wengine wa klabu hiyo kupitisha mabadiliko hayo licha ya awali kugomea.

Bi Hindu alikuwa mmoja wa wanachama ambao walikuwa wanapinga mchakato wa mabadiliko ya uendeshwaji wa timu hiyo akiwa sambamba na mmoja wa aliyekuwa kiongozi wa baraza la udhamini, Hamis Kilomoni.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Bi Hindu amesema kuwa awali alikuwa anapinga juu ya mabadiliko hayo kutokana na kutoelewa lakini baada ya kuelimishwa vizuri kwa sasa amefungua moyo wake na kumkubali Mo ambaye ndiye aliyeibuka kidedea kwenye mchakato wa kumsaka mzabuni wa klabu hiyo.

“Watu wanasema kuwa nimekubali mabadiliko haya eti kwa sababu nimepewa fedha, mimi nawaambia kwamba hakuna hata senti moja niliyopewa kwa ajili ya kulikubali hili ila ni elimu tu juu ya namna mambo yatakavyoenda ndivyo yamenifanya nibadilishe msimamo wangu,” alisema Bi Hindu ambaye alikuwepo kwenye mkutano wa mabadiliko hayo uliofanyika jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere, Posta jijini Dar.

Said Ally | Dar es Salaam

Leave A Reply