The House of Favourite Newspapers

Bi. Shakila Kuzikwa Leo Saa 10 Alasiri Charambe, Mbagala

0

1MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa taarab hapa nchini, Bi. Shakila Said aliyefariki dunia jana usiku, anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi, Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika Makaburi ya Uwanja wa Ninja yaliyopo Mbagala- Charambe jijini Dar es Salaam .

Bi Shakila alifariki ghafla jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyo wa taarabu hakuwa anaumwa wakati mauti yanamkuta.

Kwa mujibu wa familia wameeleza kuwa, taratibu zingine za mazishi zinaendelea na mwili wa marehemu ulihamishiwa hospitali ya Lugalo.

Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.

Bi Shakila aliwahi kuwika na nyimbo kadhaa ukiwemo ule maarufu, MACHO YANALIA MOYO UNACHEKA aliouimba akiwa na bendi ya JKT miaka ya 90.

Mwaka 1960, aliolewa akiwa na umri wa miaka 11 tu na kuachika akiwa na mtoto mmoja kabla ya kuolewa tena na mwanaume aliyedumu naye kwa miaka 18 na kuzaa naye watoto watano kabla ya mumewe kufariki mwaka 1975.

Baadaye aliolewa tena na mwanaume mwingine aliyezaa naye watoto watano kabla ya kuolewa tena mara ya nne na mwanaume aliyezaa naye watoto wawili. Alipokuwa na mimba ya mtoto wake wa mwisho, Shani, mume wake alimwacha. Shani alizaliwa mwaka 1993 na hapo ndipo alidai alichukia wanaume na kuamua kuishi mwenyewe.

Pamoja na kustaafu kazi JKT, Shakila aliendelea kufanya muziki na miaka miwili iliyopita alikuwa akirekodi album yake Mama na Mwana ambayo ingekuwa na nyimbo nane.

KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA

Leave A Reply