The House of Favourite Newspapers

Biashara Yatamba Kuipiga Yanga FA

0

KOCHA Msaidizi wa Biashara United, Marwa Chamberi, amesema kuwa mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Yanga utakuwa mzuri kwao na watapambana ili kupata matokeo na kutinga kwenye hatua ya fainali.

 

Timu hizo zinakutana kwenye hatua ya nusu fainali ya ASFC katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Marwa alisema: “Maandalizi yako vizuri, tunapambana ili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi yenyewe kuwa ni ya mtoano na sio ligi kwamba unatafuta pointi, kwa hiyo ni umakini unahitajika ili kuingia fainali na tunapaswa kushinda mchezo huo na utakuwa mzuri kwetu na hautakuwa mwepesi pia.

 

“Kwa upande wa bonasi sisi tunatambua kwamba hii ni kazi yetu wala sio kibarua cha ziada, ni majukumu tu ya kawaida na kila mchezaji anautumikia mkataba wake, hivyo cha msingi ni kuwa kila mechi tunaposhinda kuna posho ya ushindi.”

Stori: Na Ibrahim Mussa na Marco MzumbeDar es Salaam

Leave A Reply