The House of Favourite Newspapers

Bibi Aliyetuhumiwa Kuua Mwanafunzi Auawa Kinyama na Wananchi

MAUAJI YA KUTISHA! Tukio lisilo la kawaida limetokea Wilayani Muleba Kata ya Kishanda Mkoani Kagera ambapo mtoto mwenye Ismail Hamisi (7) ambaye alipotea tangu Aprili 5, 2019 akitokea shule, jana usiku mwili wake akiwa amefariki, umekutwa kwenye shamba la bibi mmoja akidaiwa kuufukia kwenye shimo.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wakiwa na  hasira walivamia nyumbani kwa bibi huyo na kukata migomba yake huku wakimshambulia kwa kipigo kikali na kumuua kwa kumchoma moto akiwa ndani ya nyumba yake.

 

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka Aprili 5, mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umezikwa katika shamba la bibi huyo, akiwa na sare zake za shule.

 

Aidha, Kamanda Revocatus amesema taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika.

SPIKA ALIVYOULIZA – “Kwanini MIREMBE Imejengwa DODOMA?”

Comments are closed.