The House of Favourite Newspapers

Bibi Wa Miaka 74 Auawa Kikatili Kwa Mapanga – Mbunge Shigongo Afika Kutoa Pole Kwa Familia

0

Sarah Petro (74) mkazi wa Kijiji cha Magulukwenda kitongoji cha Mizorozoro Kata ya Kalebezo wilayani Sengerema Sengerema Mkoa wa Mwanza ameuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana Septemba 22, 2024 majira ya saa mbili usiku akitokea kwa mtoto wake ambaye anaishi jirani naye.

Petro Paul ambaye ni mtoto wa Marehemu anayeishi Kijiji cha Nyehunge amesema kuwa mama yake hakuwa na ugomvi wa aina yoyote hapo kijijini anashangazwa na tukio la uonevu alilofanyiwa mama yake na kuitaka serikalia kuchukuwa hatua.

Naye, Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo alifika kwenye familia iliyopata msiba huo na kutoa pole huku akisema waviachie vyombo vya dola ili kufanya kazi yao na watu waliotekeleza mauaji hayo watakamatwa na watafikishwa kwenye mamlaka husika.

Leave A Reply