The House of Favourite Newspapers

Biden Aanza Kazi Kwa Kutengua Sera za Trump

0

RAIS  mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa.

Rais Biden tayari amesaini maagizo ya watendaji 15 yanayolenga kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Amri nyingine ni kubadilisha msimamo wa utawala wa Trump juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji.

Biden ameanza kufanya kazi katika Ofisi ya Oval baada ya kuapishwa mapema Jumatano kama rais wa 46 wa Marekani.

Kuapishwa kwa Biden kulikuwa na utofauti na nyakati nyingine yoyote kutokana na vizuizi vya maambukizi ya corona, na wachache walikuwepo kushuhudia viapo na sherehe.

Donald Trump – ambaye bado hajakubali rasmi urais kwa Biden alikataa kuhudhuria hafla badala yake alikuwa na sherehe zake binafsi katika makazi yake.

Biden ameapa kuwa rais wa Wamarekani wote sambamba na kuwa rais anayefuata sheria ya katika ya nchi huku akizitaka jamii za kimataifa kuitegemea Marekani mpya.

Watangulizi wake watatu walihudhuria shughuli ya kuapishwa kwake: Barack Obama – ambaye  Biden alikuwa makamu wake wa rais kwa miaka nane – Bill Clinton na George W. Bush,  na aliyekuwa makamu wa rais wa Trump, Mike Pence.

Sherehe za uapisho huo zilijumuisha maonyesho ya muziki  wakiwemo Lady Gaga – aliimba wimbo wa taifa – na Jennifer Lopez na Garth Brooks.

Amanda Gorman, ni mwanamashairi mdogo zaidi ambaye alighani shairi lake katika shughuli hiyo.

Katika tamasha la jioni mjini Lincoln, palitumbuizwa muziki  na Tom Hanks pamoja na Bruce Springsteen, John Legend, Jon Bon Jovi, Justin Timberlake, na Demi Lovato.

 

Ni amri zipi Biden amesaini?

Rais Biden “atachukua hatua – na si kubadili sera peke yake ya uharibifu uliofanywa na utawala wa Trump- lakini pia kuanza kuliendeleza taifa,” taarifa inayofafanua amri hiyo inaeleza.

Hii ni pamoja na mfululizo wa hatua zitakazotekelezwa kukabiliana na janga la virusi vya corona ambalo limesababisha zaidi ya vifo 400,000 nchini Marekani.

Kutakuwa na amri ya uvaaji wa barakoa na kukaa kwa umbali katiika maeneo yote ya umma.

Ofisi mpya itaweka mkakati wa kukabiliana na janga hilo la corona – kuanzia na hatua ya utawala wa Trump – kuiondoa Marekani katika Shirika la Afya (WHO).

Bomba lililofadhiliwa kibinafsi – linalokadiriwa kugharimu karibu dola bilioni 8, litakalobeba malighafi za mafuta kutoka Alberta, nchini Canada, mpaka Nebraska.

Barack Obama alipiga kura ya kuidhinisha muswada wa ujenzi wa bomba mnamo 2015 lakini uamuzi huo ulibatilishwa na Rais Trump.

Kuhusu uhamiaji, Biden amebatilisha tangazo la dharura la utawala wa Trump ambalo lilisaidia kufadhili ujenzi wa ukuta kando ya mpaka wa Mexico na pia kumaliza marufuku ya kusafiri kwa nchi nyingi za Waislamu.

Leave A Reply