The House of Favourite Newspapers

Biden: Putin Hawezi Kuitisha Marekani na NATO kwa Mikwara Yake

0
Rais wa Marekani Joe Biden

RAIS wa Marekani Joe Biden ameibuka na kudai kuwa Marekani haiwezi kutishwa na mikwara ambayo haina kichwa wala miguu inayotolewa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

 

Biden ameyasema hayo ikiwa ni baada ya Vladimir Putin kutangaza kuchukua mikoa minne kutoka katika nchini ya Ukraine huku akipiga mkwara mzito kwa mataifa ya Magharibi pamoja na Marekani.

 

Katika moja ya kauli tata alizozitoa Rais Putin ni pamoja na kusema kuwa yupo tayari kutumia nguvu ya nyuklia kulinda mikoa hiyo iliyochukuliwa kutoka Ukraine na akasisitiza pia kuwa mikoa hiyo itakuwa ni mali ya Urusi hadi mwisho wa dunia.

Rais Putin akishangilia ushindi wa kutwaa Mikoa minne ya Ukraine na kuwa ardhi ya Urusi

Naye Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kitendo kilichofanywa na Urusi cha kumega mikoa hiyo minne mali ya Ukraine ni moja kati ya matukio ya makusudi ya kuhatarisha amani na uvunjwaji wa makusudi wa sheria za usalama za Umoja wa Mataifa.

 

Katika kuonesha alama ya msisitizo Rais Putin amesema mashambulizi yoyote yale yatakayotekelezwa katika mikoa hiyo minne yatatafsiriwa ni saw ana kuishambulia ardhi ya Urusi hivyo Urusi kama nchi haitamuacha mtu salama.

 

Katika hotuba yake aliyoitoa kama majibu kwa Rais Putin, Rais wa Marekani Joe Biden ameyaita maneno ya Rais Putin kama maneno ya kipuuzi na mikwara ambayo haiwezi kuitishia Marekani na washirika wake ikiwemo mataifa ya Ulaya Magharibi.

Majeshi ya NATO

“Marekani na washirika wake hatuwezi kutishiwa na mikwara hiyo, Marekani imejiandaa vilivyo sote pamoja na washirika wetu wa NATO kulinda kila pembe ya mipaka ya nci ya Jumuiya ya NATO. Bwana Putin uelewe nimesema kila pembe ya mipaka ya NATO.” amesema Rais Biden.

 

Mikoa minne iliyotwaliwa na Urusi kutoka katika ardhi ya Ukraine ni Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhia na Kherson ambayo hadi sasa ipo chini ya utawala wa Urusi huku Rais wa Urusi Vladimir Putin akiahidi kutengeneza miundo mbinu na kuipendezesha mikoa hiyo iliyokuwa imeathiriwa na vita.

 

 

 

 

Leave A Reply