Bidhaa za Red Gold Zaweka Rekodi Ya Ubora Kwa Watumiaji

Yawezekana kwa kipindi kirefu umekuwa ukitumia bidhaa zinazozalishwa na Red Gold lakini pengine hukuwahi kujua kwamba ubora wake wa kipekee ndiyo uliosababisha zikaendelea kuwa chaguo namba moja kwa watumiaji wake karibu kila kona ya nchi.

 

Bidhaa bora zinazozalishwa chini ya brand ya Redgold, ni nyingi lakini kubwa zaidi ni Tomato Sauce, Chilli Sauce, Jam, Juice, Tomato Ketchup, Pilipili Mbuzi Sauce, Tomato Paste na Pickles na licha ya ladha bora kabisa ya bidhaa hizo, lakini pia zinatajwa kuwa na faida mbalimbali mwilini.

Miongoni mwa faida za bidhaa za Redgold zinazozalishwa na Darsh Industries Ltd ni kupunguza hatari ya saratani ya matiti, kupunguza kansa ya kibofu hatarishi, kukinga ngozi kupata madhara mbalimbali na kupunguza mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu.

 

Sababu nyingine ni kuongeza uwezo wa kuona, kuboresha afya ya mifupa na kuongeza idadi ya mbegu za kiume.

“Kwa miaka mingi nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza chipsi na mwanzo wateja walikuwa wakilalamikia tomato sauce na chili sauce nilizokuwa nazitumia lakini tangu nilipoanza kutumia bidhaa za redgold, wateja wanafurahia kwelikweli na wanazidi kuongezeka kila kukicha,” alisema Noel Joshua, mfanyabiashara wa chipsi katika eneo la Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam.

Bidhaa bora za Red Gold zinazalishwa na Kampuni ya Darsh Industries Ltd chini ya mkurugenzi wake, Mkurugenzi Mkuu Badrish Pandit na kiwanda chao kikubwa kipo katika eneo la Themi jijini Arusha, Tanzania na bidhaa zote hutengenezwa kwa mbogamboga halisi, viungo na matunda yanayolimwa chini ya uangalizi wa kitaalamu.

 

Kampuni hiyo imekuwepo nchini tangu mwaka 1999 na ubora wa bidhaa zake umesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, huku pia kikiunga mkono kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kuwaajiri wazawa na kuboresha uchumi wa viwanda nchini.

“Bidhaa zetu za REDGOLD zinazingatia sana ubora kuanzia kwenye uzalishaji wa mbogamboga, matunda na viungo vinavyotumika kutengenezea bidhaa zetu, tunazingatia thamani ya fedha anazotoa mteja wetu, virutubisho pamoja na usafi wa hali ya juu,” alisema Pandit, mkurugenzi wa kiwanda hicho.

 

Pia Darsh Industries imekuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wazawa ambapo mwaka 2016, iliingia mkataba na msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ katika kampeni yake iliyopewa jina la Ladha na Mtonyo ambapo watumiaji mbalimbali wa bidhaa hizo, walijinyakulia mamilioni ya fedha zilizotolewa kama zawadi.

“Kampuni yetu pia inafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria za nchi ambapo bidhaa zetu zote zimethibitishwa na Shirika la Ubora wa Viwango (TBS), mamlaka ya Chakula, Dawa na Vifaa Tiba (TFDA) pamoja na wasimamizi wa mazingira bora mahali pa kazi, OSHA,” aliongeza Pandit.

 

Kwa mawasiliano, unaweza kuwapata kwa kufika kiwandani kwao, Themi Industrial Area, Arusha plot namba 16 au kwa kupiga simu 0736 500 525. Unaweza pia kuwacheki kwa barua pepe, info@redgold.co.tz au tembelea website yao kwa kubofya www.redgold.co.tz.

Toa comment