Bieber Awakosoa Grammy Kuhusu Albamu Yake
MWIMBAJI wa muziki wa Pop na R&B kutokea nchini Canada, Justin Bieber, mwaka huu amepata nafasi ya kutajwa kuwania Tuzo za Grammy 2021 katika vipengele vinne ambavyo ni ‘Best Pop Vocal Album’, ‘Best Pop Solo Performance’, ‘Best Pop/Duo Group Performance’ na ‘Best Country Duo/Group Performance.’
Bieber amewakosoa waandaaji wa tuzo hizo na kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika ujumbe akielezea kushangazwa na kitendo cha waandaaji wa hao kuiweka album yake ya ‘CHANGES‘ kuwania Tuzo kwenye kipengele cha ‘Best pop vocal album’ wakati albamu hiyo ni ya R&B.
Amewataka wasitafsiri vibaya alichokisema kwani hayo ni mawazo yake ambayo mtu anaweza kukubaliana nayo au kuyakataa, pia amewashukuru watu wote waliomwezesha kutajwa kuwania tuzo katika vipengele hivyo.