The House of Favourite Newspapers

Bifu La Matola, Sven Simba Lamuibua Chama

0

MASHABIKI wa Simba wameonekana kufurahia ushindi wa tatu mfululizo walioupata kwenye Ligi Kuu Bara, lakini aliyefanikisha hilo ni kiungo mchezeshaji fundi Mzambia, Clatous Chama. Simba katika mchezo iliyopita ya ligi imepata matokeo mazuri ya ushindi katika michezo hiyo mitatu walipovaana na Mtibwa Sugar, Lipuli FC na Kagera Sugar wakitoka kufungwa na JKT Tanzania.

 

Timu yenye pointi 59 ikiongoza kwenye msimamo wa ligi leo saa kumi kamili inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na Biashara United katika mchezo wa ligi.

 

Championi Jumamosi, linakupa mkanda mzima siri ya ushindi hiyo ni kikao kikao kizito kilichofanywa kati ya viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na benchi zima la ufundi kilichowekwa kwa ajili ya kupatanishwa makocha wa timu hiyo Mbelgiji Sven Vanderbroeck na msaidizi wake, Selemani Matola.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Chama ndiye aliyewashauri viongozi hao kukutana na makocha hao kwa ajili ya kumaliza ‘bifu’ lililokuwepo awali kwenye timu hiyo la makocha hao mara baada ya mchezo wa JKT Tanzania uliomalizika kwa kufungwa bao 1-0.

 

Alisema kuwa katika kikao hicho, makocha hao walitakiwa kuvunja mabifu yao na kurejesha umoja na ushirikiano ambayo hivi sasa imerejea kwa makocha hao ambao wanashirikiana tofauti na

ilivyokuwa awali. “Amani imerejea kwenye timu hivi sasa katika timu kwa makocha haona katika kuthibitisha hilo katika michezo iliyopita ya ligi ambayo yote imeshinda Matola ndiye aliyepanga ni baada ya Sven kumpa nafasi ya yeye kupanga kikosi cha kwanza.

 

“Kitu hicho awali hakikuwepo, kwani kocha Sven alikuwa hataki ushauri wa mtu yeyote kutoka kwenye benchi la ufundi na badala yake kila kitu alikuwa akifanya yeye, lakini katika kikao hicho cha viongozi kocha huyo alibadilika na kufanya kazi kwa kushirikiana.

 

“Lakini aliyesababisha hayo yote ni Chama ambaye yeye aliwashauri kufanya kikao na benchi la ufundi baada ya kutoka kufungwa na JKT Tanzania, kama siyo yeye basi bifu lingeendelea kwa makocha hayo,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Senzo Masingisa hivi karibuni alithibitisha kumalizika kwa bifu hilo la makocha hao akisema kuwa: “Kilichotokea kwa makocha wetu ni kitu cha kawaida ambacho popote kinatokea, ilitokea hali ya kutoelewana lakini hivi sasa kila kitu kipo poa baada ya kufanya kikao na makocha hao.”

 

 

 

Leave A Reply