Bifu La Nandy, Ruby Kwisha!

Faustina Charles ‘Nandy’.

KUTOKANA na madai ya hapa na pale kwamba wasanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na msanii mwenzake, Hellen George ‘Ruby’ wana bifu zito, hatimaye bifu hilo linadaiwa kuzimwa baada ya Ruby kuonekana akiimba nyimbo za Nandy.

Hellen George ‘Ruby’.

Siku chache zilizopita, Ruby alionekana akiwa kwenye ‘interview’ ya kituo kimoja cha redio akiimba Wimbo wa Kivuruge ya Nandy, kisha baada ya muda Nandy akaposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumsifu kwa uimbaji wake, jambo lililozua gumzo na kudhihirisha kuwa sasa hakuna tofauti baina yao.

 

Kutokana na ishu hiyo, Ruby alipotafutwa simu yake haikuwa hewani, kwa upande wake Nandy alisema; “Nimefurahi mno Ruby kuimba wimbo wangu, anajua, ujue sisi hatujawahi kuwa na bifu hayo yanazushwa na mashabiki, tarajieni kuona makubwa huko mbeleni, sababu tunafanya kazi sehemu moja hata tukiamua kufanya kolabo kama mashabiki wanavyotushauri ni sekunde tu, ila suala hilo siwezi kuliongelea sana kwa sasa

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment