The House of Favourite Newspapers

Big Brother Naija; Ni Vita na Mapenzi Mjengoni, Chichi na Diana Wawashiana Moto

0

 

MAMBO yanazidi kupamba moto ndani ya mjengo wa Big Brother Naija ‘Level Up’ ambapo mapenzi na ugomvi wa hapa na pale kati ya washiriki, vimeendelea kuchukua nafasi kila kukicha.

Katika tukio la hivi karibuni, washiriki wawili wa kike, Chichi na Diana almanusra wazichape mjengoni humo ambapo waliingia kwenye mzozo mkubwa na kutoleana maneno machafu kabla ya kuamuliwa.

 


Chanzo cha vita kati yao, ilikuwa ni ishu ya mapenzi, wakimgombea Deji. Utata ulianza baada ya washiriki kutoka mjengo mwingine kuchanganywa kwenye ‘Level Up’ ambapo Deji alionesha ukarimu usio wa kawaida kwa Diana, jambo ambalo lilimkasirisha Chichi ambaye amekuwa naye karibu kwa muda mrefu.

Hasira zaidi zilimpanda Chichi baada ya kuwasikia Diana, Allysyn na Doyin wakimzungumzia Dejin, ndipo alipowavamia na mojamoja akamvaa Diana na mzozo mkubwa ukaibuka kati yao ingawa baadaye walisuluhishwa na kuelewana.

Mashindano ya Big Brother Naija yanaoneshwa moja kwa moja na DSTV Chaneli namba 198 na 199 ambapo mashabiki kutoka kona zote za Bara la Afrika, wanaendelea kushuhudia kila kinachoendelea kwenye mjengo huo.

Leave A Reply