The House of Favourite Newspapers

Bil 2.5 Zatengwa Kufanya Usajili Yanga

0

KATIKA kuhakikisha wanatengeneza kikosi chenye hadhi na tishio katika michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara msimu ujao, Yanga wametenga Sh 2.5 Bil kufanikisha usajili wa wachezaji wapya.

 

Yanga hadi hivi inahusishwa kusajili baadhi ya wachezaji akiwemo Shaban Djuma (AS Vita), Denis Kibu (Mbeya City), Dickson Ambundo (Dodoma Jiji) na David Bryson (KMC).

 

Pia timu hiyo ipo katika mazungumzo na Lazaros Kambole, Anthony Akumu (Kaizer Chiefs), Mercey Ngimbi (Miniema FC), Ben Malango (Raja Casablanca) na Ferjan Sassi (Zamalek).

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, bajeti hiyo ya Sh 2.5Bil itawahusisha wachezaji wa kigeni na wazawa ambao Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia, amewapendekeza.

 

Mtoa taarifa huyo alisema, imetengwa bajeti hiyo kubwa kwa ajili ya kuhakikisha wanawasajili wachezaji wote waliokuwepo katika mipango yao ikiwemo kuwavunjia mikataba katika klabu zao.

 

Aliongeza kuwa, tayari fedha hizo zimeanza kutumika katika kuwasajili wachezaji akiwemo Djuma aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru.

 

“Kikubwa tumedhamiria kuirudisha Yanga kwenye hadhi yake na ili irejee ni lazima tufanye usajili bora utakaoendana na ukubwa wa timu yetu katika msimu ujao.

 

Hivyo tumetenga kiasi cha Sh 2.5Bil kwa ajili ya kusajili wachezaji wote waliokuwepo katika mipango yetu ili kuhakikisha tunakuwa na kikosi kipana kitakacholeta ushindani msimu ujao.

 

“Fedha hiyo ishaanza kutumika katika usajili baada ya kuchukua baadhi ya wachezaji wa kigeni na wazawa kwa siri tukihofia kuingiliwa na timu nyingine,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema: “Mapema kuzungumzia suala hilo la bajeti ya usajili ya timu na kingine ni vigumu kuiweka siri wazi na kila mtu aione, kikubwa tumepanga kufanya usajili wa kisasa utakaoendana na hadhi yetu.”

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar

RONZE Baada ya KUACHANA na SHILOLE Afunguka – “HANISAPOTI, ZUCHU na IBRAAH, MIMI MKUBWA Kuliko WAO”

Leave A Reply