The House of Favourite Newspapers

Bil.6.7 Zaboresha Zaboresha Sekta Ya Elimu Muheza

0

Takribani shilingi bilioni 6.7 zimetumika katika ujenzi wa shule za sekondari 10 katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shule hizo zimejengwa katika kata 10 kati ya 13 za wilaya hiyo ili kusogeza huduma  kwa wakazi wa maeneo hayo ambao watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kwaajili ya masomo sababu iliyokuwa inasababisha matokeo mabaya katika mitihani ya Elimu ya sekondari.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba katika uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho iliyolenga kuibua  vipaji vya watoto na kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga na mgeni rasmi akiwa Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati.

“Hapo awali kulikuwa na kata 13 ambazo hazikuwa na shule za sekondari lakini  alivyoingia madarakani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaleta fedha ambazo  zimejenga shule za sekondari katika kata 10 na mwaka huu wa bajeti kuna kata  nyingine ya Kwezitu ambayo na yenyewe imeletewa milioni 580 kwaajili ya kujenga  shule ya sekondari na tafsiri yake ni zimebaki kata mbili tu” Amesema

Katika Hatua nyingine Katimba amempongeza Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ kwa kushirikiana na rafiki zake ambao wamejenga shule yenye madarasa sita,vyoo na Ofisi katika kata ya Magoroto ambayo mwaka 2025 itaanza kupokea wanafunzi.

Amesema serikali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa  mafunzo kwa walimu ya kuwajenga uwezo na kujenga nyumba za kuishi ili waweze kufanya kazi kwa bidii na ubunufu katika sekta ya elimu.

 

Akizungumzia mafanikio katika sekta ya Elimu katika Jimbo la Muheza,mbunge wa  Jimbo hilo Hamis Mwinjuma amesema ndani ya miaka mitatu jumla ya vyumba vya madarasa 212 vimejengwa na amemshukru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka alama ya upatikanaji wa Elimu katika wilaya ya Muheza.

Akihutubia wananchi wa Muheza waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho Naibu Waziri Mkuu na Waziri na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amehimiza wazazi na walimu kushirikiana katika kuwaandaa watoto ili kupata viongozi wa baadae.

”NIMEKATA TAMAA MPAKA NATAKA NIUZE FIGO YANGU” – MAGE MIAKA 24 ALIYEJIKUTA ANAISHI KAMA KICHAA DAR

Leave A Reply