The House of Favourite Newspapers

Bilionea Amchumbia Mariah Carey

0

mariaMariah Carey na James Packer.

DIVA wa muziki duniani, Mariah Carey amepanga kuolewa na bilionea maarufu wa Australian, James Packer.

Hii imedhihirika juzi usiku baada ya Packer, mwenye umri wa miaka 47, kumvisha pete ya almasi (yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.5) mwanamama Carey, mwenye umri wa miaka 45, tukio likifanyika mbele ya umati wa marafiki wa karibu wa Carey wakati wa chakula cha usiku kwenye mgahawa wa Eleven Madison Park  huko New York.

Wapenzi hao wamekuwa katika mahusiano kwa takribani mwaka mzima sasa tangu waliopokutana kwa mara ya kwanza mwaka 2014 kupitia rafiki wa Packer Brett Ratner hyuko Aspen, walianza kuwa marafiki wa kawaida na baadaye wakawa wapenzi.

Mariah carey (2)Kabla ya wawili hao kukutana kimahusiano, kwa nyakati tofauti Carey aliwahi kuolewa na Nick Cannon na Tommy Mottola, kwa upande wake Packer aliwahi kumuoa Jodhi Meares na Erica Baxter kwa nyakati tofauti pia.

Carey anawatoto mapacha wawili wenye umri wa miaka minne Moroccan na Monroe aliyowazaa na Cannon, wakati Packer ana watoto watatu Indigo, Jackson na Emmanuelle.

Taarifa za uuhusiano wa Carey na Packer ulianza kufahamika zaidi June mwaka jana baada ya kunaswa wakila wakijiachia kimahaba kwenye visiwa vya Capri huko Italia wakati huo Carey alikaririwa akisema ndoa yake na cannon haikuwa na furaha bali mateso.

 

#pipmoments

A photo posted by Mariah Carey (@mariahcarey) on

Leave A Reply