Bilionea Jack Ma Aachia Ngazi Kampuni za Alibaba

SHANGHAI (Reuters) — Mwenyekiti na mwaznilishi wa Makampuni ya China yaa Alibaba Group, Jack Ma, ameachia ngazi katika kampuni hilo la Chinaese jana (Jumanne) akimwachia Daniel Zhang kuwa mrithi wa jukumu kubwa la kuimarisha shughuli za kampuni hilo kubwa lenye utajiri wa dola bilioni 460 ambapo sasa linayumba.

 

Wakati  Ma, aliyetimiza umri wa miaka 55 jana, na aliyeng’ara katika hafla ya kumuaga katika Kituo cha Michezo cha Olimpiki chenye uwezo wa kuingiza watu 80,000 cha Hangzhou ambapo palikuwa na muziki wa kumwaga na watu maarufu kibao, watu waliohudhuria walitegemea picha ambavyo kampuni ya Alibaba itakavyokuwa chini ya Daniel Zhang.

 

Akiwa ni mhasibu na mwenye kuongea polepole, Zhang  yuko tofauti  na Ma ambaye uongozi wake wa kuvutia ulimfanya kuwa mjasiriamali maarufu tangu alipoianzisha kampuni hiyo miaka 20 iliyhopita jijini Hangzhou mashariki mwa China.

“Ana uwezo, maono  na maarifa makubwa kama kompyuta ya hali ya juu katika kuendesha biashara sasa na siku zijazo,” Ma anamwelezea Zhang katika ujumbe wa kumteua katika nafasi yake mwaka 2018.

 

Moja ya changamoto za Zhang itakuwa kutafuta maeneo mapya wakati sekta ya biashara ya China inapozidi kukua, anasema mchambuzi mmoja.

“Iwapo Alibaba inataka kupata ubunifu mpya, hili litakuwa jambo gumu zaidi kuliko zamani,” alisema Liu Yiming, mchambuzi katika kampuni la teknolojia akiongeza kwamba:  “Kwa Daniel Zhang, hii itakuwa changamoto kubwa.”

 

Mauzo ya rejareja ya China kwenye mtandao yalikua kwa asilimia 17.8 tu katika nusu ya kwanza ya mwaka 2019, ikiwa karibu nusu ya ongezeko la asilimia 32.4 mwaka uliopita, kwa mujibu wa takwimu za taifa.

Kujiuzulu kwa Ma kulikotangazwa mwaka jana kulichukuliwa kuwa si jambo la kawaida, kwani ni adimu kwa mwasisi wa kampuni kubwa kama hilo kustaafu mapema hivyo.

 

Chini ya uongozi wa Ma, Alibaba imekua na kuwa kampuni imara zaidi ambapo lina mtaji wa dola bilioni 460.  Isitoshe, lina wafanyakazi zaidi ya 100,000 likiwa limejitanua katika huduma za kifedha na kompyuta.

Baada ya kustaafu kwake, Ma — mtu tajiri zaidi nchini China akiwa na utajiri wa dola bilioni 38.4, kwa mujibu wa jarida la Forbes — atatumia muda mwingi zaidi katika kutoa misaa na elimu sehemu mbalimbali.


Loading...

Toa comment