The House of Favourite Newspapers

Bilionea wa Japan Yusaku Maezawa Ataja watu wanane Atakao kwenda nao Kwenye Safari ya Kwenda Mwezini

0
Bilionea wa Japan Yusaku Maezawa.

Bilionea wa Japan Yusaku Maezawa amewataja watu wanane wenye bahati ya mtende atakao kwenda nao kwenye safari ya kwenda mwezini kwa kutumia chombo cha SpaceX Starship ya Elon Musk mwaka ujao bure bila malipo yoyote.

Maezawa, 47, ambaye alisafiri kwa ndege hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kwa kutumia chombo Soyuz ya Urusi kama mtalii mnamo 2021, anatarajia kurudi angani na kuzunguka kwenye mwezi kama sehemu ya mradi unaoitwa dearMoon.

Safari yao inapaswa kudumu karibu wiki nzima na kutua kwenye satelaiti ya Dunia haijajumuishwa katika mpango wake.

Mfanyabiashara huyo wa Kijapani ambaye alianzisha duka la nguo la mtandaoni Zozo alinunua viti vyote kwenye chombo Starship, na kinapaswa kwenda mwezini wakati wa 2023.

Mnamo Machi 2021, Maezawa alitangaza wito wa maombi ya “tiketi” nane kwa wanaotaka kwenda kwenye mwezi, na sasa ametaja majina ya wale aliowaona kuwa wanastahili kwenda naye.

1. Steve Aoki -DJ na mtayarishaji vipindi (USA)
2. Tim Dodd – Nyota wa YouTube, mwandishi wa blogu ya anga za juu ya Everyday Astronaut (USA)
3. Yemi Akinemi Dele (Yemi AD) – Mpangaji dansi, mwigizaji, msanii (Czech Republic)
4. Rhiannon Adam – mpiga picha (Ireland) (mwanamke pekee katika timu ya wafanyakazi kuu)
5. Karim Ilia – Mpiga picha (Uingereza)
6. Brandln Hall – Mwongozaji wa filamu (USA)
7. Dev Joshi – Mwigizaji wa filamu (India)
8. Choi Seung Hyun (TOP) – Nyota wa kundi la muziki la K-Pop Star (Korea Kusini)

Leave A Reply