The House of Favourite Newspapers

Bilioni 1.8 zamwagwa usajili Yanga

0

YANGA imeweka rekodi kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara katika usajili, ikisajili wachezaji 20 katika madirisha mawili ya usajili huku watani wao Simba wakisajili 10 pekee. Achana na rekodi hiyo, nyingine Yanga imebadili mabenchi ya ufundi mara tatu mfululizo ndani ya msimu mmoja.

 

Walianza na Mkongomani Mwinyi Zahera ambaye alisitishiwa mkataba, akaletwa Charles Mkwasa kukaimu kabla ya Mbelgiji Luc Eymael kuchukua nafasi yake.

Lakini kikubwa zaidi, katika usajili wa wachezaji 20, Yanga itajikuta inatumia bilioni 3 katika kuwahudumia wachezaji ambao hadi sasa wengi wao wanaonekana hawana msaada uliotarajiwa.

 

Kwa wachezaji waliosajili dirisha kubwa, Metacha Mnata alisajiliwa Sh Mil 30. Analipwa mshahara wa Sh Mil 3, hivyo kwa miaka miwili aliyosajiliwa, atachukua jumla ya Sh Mil 72.

Lamine Moro alisajiliwa naye kwa dau la Sh Mil 30. Analipwa mshahara Sh Mil 5.5, kwa mkataba wa miaka miwili aliyosajiliwa atajikusanyia Sh Mil 180.

 

Abdulaziz Makame, alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 30. Analipwa mshahara wa Sh Mil 2, kwa mkataba wake wa miaka miwili atakayoichezea Yanga atachukua Sh mil 48.

Maybin Kalengo aliyesajiliwa dirisha kubwa yeye alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 30. Alikuwa anachukua mshahara wa Sh Mil 3, lakini tayari ameshasepeshwa akiwa ameshalipwa mshahara wa zaidi ya miezi 6 Sh mil 18.

 

Sibomana alisajiliwa kwa dau la Sh mil 30. Anachukua mshahara wa Sh Mil 3, kwa muda wa miaka miwili kama atamaliza, atachukua Sh mil 72.

Sadney Urikhob alisajiliwa kwa dau la Sh Mil. 30. Anachukua mshahara wa Sh mil 3, tayari ameshasepeshwa.

 

Juma Balinya alisajiliwa kwa dau la Sh 30m. Anachukua mshahara wa Sh Mil 3, naye alishaachana na timu hiyo.

Issa Bigirimana alisajiliwa kwa dau la Sh mil 30. Anachukua mshahara wa Sh mil 3 kwa miaka miwili aliyosajiliwa ilikuwa achukue kitita cha Sh mil 72 lakini alikomba Sh 18m kwa miezi sita.

 

David Molinga alisajiliwa dau la Sh Mil 30. Anachukua mshahara wa Sh Mil 3, kwa miaka miwili atakayoichezea Yanga atachukua Sh Mil 72.

Ally Mtoni ‘Sonso’ alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 20. Anachukua mshahara wa Sh Mil 2, kwa miaka miwili aliyosaini atachukua Sh Mil 48.

 

Mapinduzi Balama alisajiliwa kwa dau la Sh Mil Anachukua mshahara wa Sh Mil 2, kwa miaka miwili aliyosaini Yanga, jumla atachukua Sh Mil 48.

Moustafa Selemani alisajiliwa kwa Sh Mil 20, Anachukua mshahara wa Sh Mil 2, kwa mkataba wake wa miwili jumla atachukua Sh Mil 48.

 

Mwalami Issa ‘Marcelo’ naye alisajiliwa kwa dau la Sh mil 20. Analipwa mshahara wa Sh Mil 2, kwa miaka miwili ataka yocheza Yanga atachota Sh Mil 48.

Farouk Shikalo alisajiliwa kwa dau la Sh mil 50. Anachukua mshahara wa Sh mil 3, kwa kipindi cha miaka miwili alichosajiliwa atachukua Sh mil 72.

 

Tariq Seif alisajiliwa kwa dau la Sh Mil Anachukua mshahara wa Sh Mil 2, kwa mkataba wa miaka miwili atakaouchezea Yanga atachukua Sh Mil 48.

Adeyum Saleh alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 20. Anachukua mshahara wa Sh mil 2, kwa mkataba wake wa miaka miwili Yanga atachukua Sh Mil 48.

 

Ditram Nchimbi yeye alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 30. Analipwa mshahara wa Sh Mil 2, kwa mkataba wa miaka miwili ataondoka na Sh Mil 48.

Yikpe Gnaimen alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 30. Analipwa mshahara wa Sh Mil 3, kwa mkataba wa miaka miwili atachukua Sh 72m.

 

Mnyarwanda Haruna Niyonzima alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 60. Analipwa mshahara wa Sh Mil 6, kwa mkataba wa miaka miwili atachukua Sh Mil 144.

Mghana Bernard Morrison naye alisajiliwa kwa dau la Sh Mil 60. Analipwa Sh Mil 6, kwa mkataba wa mwaka mmoja aliosaini atajibebea Sh Mil 72.

 

Fedha hizo za usajili na mishahara, zinaigharimu Yanga jumla ya Sh bilioni 1.8 na ushee, hasa kama wachezaji wote watamaliza mikataba lakini hata wengi wao wakiachwa, tayari kuna gharama kubwa zitakuwa zimetumika kwa ajili ya huduma yao.

 

Wachezaji hao wote walisajiliwa katika msimu huu wa ligi chini ya uongozi wa Dk Mshindo Msolla na makamu wake Frederick Mwakalebela aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

 

Akizungumzia usajili na gharama hizo, walizozitumia Yanga, Mwakalebela alisema: “Katika msimu huu tumetumia gharama kubwa za usajili kutokana na idadi kubwa ya usajili na hiyo ni baada ya kumuamini aliyekuwa kocha wetu kusimamia usajili wote na kujikuta tukisajili baadhi ya wachezaji wasiokuwa na umuhimu katika timu.

 

“Na hilo lilionekana wazi tulisajili washambuliaji wengi tukiamini wataipa mafanikio lakini mwisho wa siku wamekuja kuiua timu ambao wote katika usajili wa dirisha dogo tuliwaacha mfano Balinya (Juma), Bigirimana (Issa), Sadney (Urikhob) na Kalengo (Mybin) lakini kama tungefanya usajili vizuri katika usajili mkubwa basi tusingesajili idadi hiyo ya wachezaji.”

Leave A Reply