The House of Favourite Newspapers

Bilioni 1 Ya Mo..Unakula bata la laki kila siku miaka 27

Mohammed Dewji ‘Mo’.

 

UKIMUIBUA Mohammed Dewji ‘Mo’ alipo unajishindia Sh bilioni 1 kwa mujibu wa familia ya muwekezaji huyo wa Simba. Kimchanganuo fedha hiyo ni Sh milioni 1000. Mwanachama huyo wa Simba alitekwa Alhamisi iliyopita wakati akiingia mazoezini kwenye Hoteli ya Colloseum jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana.

 

Mchanganuo uliofanywa na Championi Jumatano, umebaini kwamba kama ukishinda dau hilo, kwa matumizi ya kawaida ya Sh 100,000 kwa siku, unaweza kula bata kwa miaka 27 na chenji inabaki.

Lakini vilevile ukiamua kukufuru na kutumia Sh milioni moja kila siku, utakula bata miaka miwili na ushee. Lakini kama ukifanya matumizi ya Sh 100,000 kwa miaka hiyo 27 itakuwa ni siku 9855 ambazo utakuwa umetumia Sh mil 985.5 ambapo inamaanisha zitakuwa zimesalia Sh 14,500,000 itimie bilioni.

 

MFANO Kama ukishinda dodo hilo la bilioni moja unaweza kuishi kwa mchanganuo huu kila siku ya Mungu kwa miaka 27; Usafiri; matumizi ya kawaida kabisa ya usafiri yanaweza kufikia Sh10,000 kwa matumizi ambayo yanaweza kuwa usafiri binafsi au bodaboda na Bajaj. Chai; Ni Sh 5,000 kwa kila asubuhi. Hii wakati mwingine inaweza kuwa supu na soda, juisi au maji.


Vocha; Matumizi ya vocha kwa siku ni Sh10,000. Cha mchana; Msosi wa mchana na mazagazaga yake yanaweza kufikia Sh15,000 kwa siku. Viburudisho; Iwe mchana au usiku baada ya mihangaiko makadirio ya viburudisho tumekadiria ni Sh 30,000 hata ukiwa na marafiki.

 

Familia; Hata ukiwa na familia ambayo inakulazimu kuacha fedha ya matumizi nyumbani kila kukicha una uhakika wa kuwapa Sh 30,000 na mtoto aliyezaliwa leo akafikisha miaka 27 na akapata ajira na mkwanja ukiwepo

Stori na Philip Nkini, Dar es Salaam | Championi Jumatano

Comments are closed.