The House of Favourite Newspapers

Billnas amkana Nandy kweupe

0

MKALI wa Bongo Fleva anayekimbiza na Ngoma ya Mafioso, William Lymo ‘Bilnass’ amemkana kweupe mwanadada Faustina Charles ‘Nandy’ kuwa hana mpango wa kufunga naye ndoa.

 

Juzikati, kwenye moja ya intavyu zake, Nandy alikaririwa akisema kuwa atafunga ndoa mwaka 2021 na alipoulizwa kama atafunga na Bilnass, alikuwa na kigugumizi.

 

Bilnass au Bilinenga ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, hakuna kinachoendelea kati yake na Nandy na kwamba kwa sasa amebaki kuwa kama mwanamuziki mwenzake.

 

“Hakuna kitu kama hicho. Ni kweli nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini siyo na Nandy,” amesema Bilnass ambaye uhusiano wake wa kimapenzi na Nandy ulibumburuka baada ya kusambaa kwa video yao chafu wakiwa chumbani.

HAPPYNESS MASUNGA

Leave A Reply