The House of Favourite Newspapers

Bin Kleb, Ndama wazuia dili la Ajibu Simba


KAMATI mpya ya Kuhamasisha Uchangiaji wa Fedha ya Yanga ambayo Abdallah Bin Kleb (pichani)na Ndama Mtoto wa Ng’ombe ni miongoni mwa vigogo, imezuia uwezekano wa Ibrahim Ajibu kurudi Simba.

 

Hiyo ina maana kuwa kama ishu zitakaa sawa, Ajibu ataendelea kuwepo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambao inaelezwa kuwa baadhi ya vigogo wa Simba walikuwa wakijaribu kumshawishi.

 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anthony Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu amependekeza Zahera na Ajibu kuendelea kubaki watia saini kwenye akaunti yao ya benki na kama kuna ishu zake ndogondogo zitawekwa sawa.

Ibrahim Ajibu akifanya yake.

Ten ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliwataja wengine watakaokuwepo katika orodha ya watia saini yeye Mwenyekiti Mavunde na makamu wake pamoja na mhasibu, kiongozi kutoka kwenye sekretatieti ya timu hiyo.

 

“Uongozi kupitia kamati hii ya Mavunde ipo kwenye mikakati mizuri kuhakikisha klabu inavuka kwenye kipindi hichi kifupi wakati ikielekea kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi na mabadiliko mengine”

 

“Tukumbuke fedha hizi zinakusanywa maalumu kwa ajili ya usajili na mambo mengine yenye manufaa kwa klabu kwa mujibu wa mahitaji ya kocha wetu atakayoyatoa katika usajili wake atakaoupendekeza kwenye msimu ujao

 

“Kamati hiyo tayari imeweka malengo yake ya kuchangisha Shilingi Bilioni 1.5 itakayotumika kwa ajili ya usajili na lengo ni kuisuka timu nzuri itakayokuwa na ubora na ushindani wa kitaifa na kimataifa.

 

“Hivyo, kamati hiyo imependekeza na kupitisha kuwabakisha Zahera na Ajibu kuendelea kuwa watia saini katika akaunti yetu ya benki itakayotumika kuchangisha fedha,”alisema Ten

Comments are closed.