Larry Gomes anajulikana zaidi kama binadamu mbweha. Zaidi ya 98% ya mwili wake wote umefunikwa na manyoya, ndiye anashikiria rekodi ya dunia ya guinness ya kuwa binadamu mwenye nywele nyingi zaidi akiipata Feb 2000, yeye pamoja na ndugu zake watatu.
Alizaliwa na tatizo la kurithi linaloitwa hypertrichosis ambalo huathiri namba 1sana ya watu duniani, huku takwimu za watu waliothibitika kuzaliwa na shida hii tangu karne ya 19 wakiwa hawafikii 100 duniani. Gomez ameoa mwanamama anayefahamika kwa jina la Alicia Martines.
Tatizo hili hutokea siku za mwanzo kabisa za utungwaji wa mimba lakini pia linaweza kutokea wakati wowote wa uhai wa binadamu (japo ni nadra sana). Hata hivyo, hypertrichosis hadi sasa haina tiba ya kudumu zaidi ya njia za kupunguza ukubwa wa tatizo kama vile kunyoa, bleaching, trimming, waxing na chemical depilatories.