The House of Favourite Newspapers

BINTI ADAIWA KUUAWA KWA RISASI NA ASKARI, MAMA YAKE AJERUHIWA

Neema Dominick mkazi wa Kigamboni Mtaa wa Tuamoyo jijini Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la paja na askari Magereza. Baada ya risasi iliyomuua Neema kutokea upande wa pili pia ilimjeruhi mama yake mzazi, Rehema Ibrahimu katika eneo la paja.

 

Mauti hayo yalimpata Neema jana akiwa nyumbani kwao karibu na Mahakama ya Kigamboni wakati askari wa Magereza alipokuwa akijaribu kumzuia mtuhumiwa asitoroke mahakamani. Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu, Juma Mwinjaku alisema kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka kwa mara ya kwanza askari wakafanikiwa kumdhibiti kabla ya kutoroka tena na kuamua kutumia risasi kumzuia.

 

“Mara zote alipotoroka alikuwa akitumia upande ambao nyumba yetu ipo jambo ambalo lilifanya hata walipotumia risasi kuwa rahisi kutufikia.”

“Lakini kwa nini watumie risasi kumzuia mtuhumiwa ilhali wanajua eneo lile liko karibu na makazi ya watu pamoja na shule? Kwa nini hawaangalii madhara yanayoweza kutokea kwa watu,” alihoji.

“Binti huyo alimaliza kidato cha nne mwaka juzi kuna wakati alikuwa akitaka kwenda jeshini akakosa nafasi hivyo alikuwa yupo nyumbani tu akisubiri utaratibu mwingine,” alisema.

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa aliyekuwa akizuiwa kwa risasi alikuwa tayari ameachiliwa na Mahakama.

VIDEO: SAKATA LA SUGU, CHADEMA WAWATAKA POLISI WASIKURUPUKE

Comments are closed.