The House of Favourite Newspapers

Binti Aliyepata Scholership India Arudi Na Ugonjwa Mwaka 1 Kabla Ya Kuhitimu – Video

 

Ni huzuni kwa Leyla Shabani Mrosa (23), msichana mwenye ndoto kubwa aliyefanya vizuri kwenye masomo hadi kupata scholarship ya kusomea Udaktari nchini India.

Akiwa njiani kutimiza ndoto zake, Leyla alikumbwa na ugonjwa ghafla, hali iliyomlazimu kusitisha masomo na kurejea Tanzania kwa ajili ya matibabu.

Kwa sasa, Leyla hawezi kusimama wala kukaa, mikono yake haina nguvu, na hutumia ulimi wake pekee kuendesha simu kwa ajili ya kujisomea na kutafuta msaada.

Amekuwa kitandani kwa takribani miaka mitatu, lakini bado ana matumaini ya kupona na kurejea katika safari yake ya elimu.

Tuungane kumsaidia Leyla apate matibabu yanayoweza kumbadili maisha! Mchango wako unaweza kuwa mwanga wa kurudisha ndoto zake.

Wasiliana na mama yake mzazi kwa msaada wowote:
📞 0679282279
📞 0756809334 (Nuru Jumbe)