The House of Favourite Newspapers

BINTI ATESEKA MIAKA 6 KITANDANI – VIDEO

MATESO gani haya? Ndivyo unavyoweza kusema ukisikia mateso na maumivu makali ya miaka sita aliyopitia mwanamke Adelina Peter (26), mkazi wa Yombo-Kilakala jijini Dar es Salaam.

Adelina anakesha na kushinda kila siku akilia kutokana na kusumbuliwa na nyonga ambayo imemfanya mpaka mguu wake mmoja kuonekana mfupi kuliko mwingine.

 

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa ambalo limejitolea kuwasaidia watu mbalimbali wenye shida hasa matatizo ya kiafya ili wachangiwe, Adelina anasema kuwa tatizo lake hilo lilianza tangu akiwa na umri wa miaka kumi, lakini lilianza kumlaza kitandani akiwa na umri wa miaka 20 hadi sasa ana 26.

 

Adelina anasema alianza kwa kuumwa tu mguu mmoja, lakini siku zilivyozidi kusonga ukahamia mguu mwingine ambao nao ulianza kuumwa.

 

“Nilipoanza kuumwa mguu mmmoja nilijua wazi kuwa ninaumwa halafu nikitumia dawa za kawaida, nitapona tu na nitakuwa sawa, lakini haikuwa kama nilivyokuwa ninafikiria kwani tatizo lilizidi kunitesa kila kukicha,” anasema Adelina.

Anaendelea kusema kuwa, baada ya mguu huo kuendelea kuuma, ulianza kutoa usaha chini ya nyayo maana kulitokea kama malengelenge.

Anasema alianza kupelekwa kwenye matibabu Hospitali ya Temeke jijini Dar) kisha Muhimbili.

 

Anasema kote huko walihitaji fedha na hana uwezo hivyo kukosa namna na kuondokana na maumivu hayo.

“Kuna wakati mimi na mama yangu tunajifungia ndani tunalia sana kwa sababu hatujui kwa nini nimekumbwa na tatizo hili kwa sababu mguu unaniuma hadi nimekuwa mdogo kabisa.

“Nimekuwa ni mtu wa kulala tu, siwezi kukaa, wala kutembea. Mimi ni wa kulala tu hadi sasa nimelala miaka sita kitandani,” anasema Adelina huku akilia kwa uchungu.

 

Adelina aliongeza kuwa, anatamani sana kwenda hospitalini ajue tatizo lake ni nini kiundani, lakini hana fedha. Yeye na mama yake wanaishi maisha ya shida mno huku mama yake ndiye amekuwa akihangaika kwa kila kitu yeye akiwa hajiwezi hata kuamka hapo alipo.

“Yaani maumivu ninayoyasikia siwezi kuelezea, naumwa mno, nimekataa tamaa, ninahitaji kwenda hospitalini nipate matibabu, lakini sina uwezo wowote,” alisema Adelina.

Mtanzania mwenzetu, kama umeguswa na tatizo ambalo linamkabili Adelina, msaidie kupitia namba yake ya simu ya mkononi 0689 246 937.

Stori: IMELDA MTEMA

Msikilize Akisimulia kwa Uchungu

Comments are closed.