Binti: Nauawa Muda Wowote!

Samra Halfani akisimulia yaliyomkuta.

ROHO Mkononi! Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Samra Halfani, mkazi wa Mbagala- Kizuiani jijini Dar, yupo kwenye wakati mgumu akihofia kuuawa muda wowote baada ya kupewa kibano kikali na njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la moja la Omari.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Samra alisema kuwa, siku hiyo, akiwa nyumbani, alimsikia mama yake mdogo akipiga kelele chumbani hivyo haraka alikimbilia kwenda kuangalia kilichomsibu.

Akioyesha makovu.

 

Alisimulia kilichomkumba baada ya kukimbilia chumbani kwa mama yake mdogo huyo:

“Nilipoingia tu, nikamkuta Omari amemkaba mama mdogo, nilipojaribu kwenda kumnasua mama mdogo alikimbia ndipo ugomvi ukahamia kwangu.

“Huyo jamaa alinikamata na kuanza kunishambulia kwa ngumi na mateke wakati mwingine nilipojaribu kujitetea, alinikaba shingoni almanusura anitoe roho.

Akilia.

 

“Limjamaa lina minguvu sana maana walikuja watu kutaka kuniokoa, lakini wote aliwazidi nguvu na kuwaambia atahawahamishia ugomvi huo kwao hivyo wengi wakanywea na kuniacha nikiendelea kupigwa.

“Hata hivyo, baadaye wasamaria wema waliongezeka na kuweza kumdhibiti ndipo nikachoropoka na kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mbagala Kizuiani kutoa taarifa maana aliapa lazima aniue muda wowote.

 

“Nilipofika polisi niliwaeleza kuwa kuna mtu ananitishia kuniua ambapo walinipa fomu namba tatu ya polisi PF-3 kwa ajili ya kwenda kutibiwa ambapo waliniambia baada ya kutibiwa nilirudi kwa ajili ya kufungua kesi.

“Niliporudi nilimfungulia kesi njemba huyo kwenye jalada lenye namba MBL/ RB/2399/2018- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI NA KUTISHIA KUUA.”

Mwanahabari wetu alimtafuta njemba huyo kwa njia ya simu ambapo simu yake ilikuwa haipatikani hadi Jumamosi iliyopita.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Mambosasa: Abdul Nondo Alikwenda Iringa kwa Mpenzi Wake