The House of Favourite Newspapers

Binti wa Paul Walker aishtaki Porsche

0

Paul Walker

Paul Walker enzi za uhai wake.

BINTI wa staa wa filamu za ‘Fast and Furious’, Paul Walker ameishtaki kampuni ya kutengeneza magari ya Porsche kufuatia ajali iliyopelekea kifo cha baba yake mwaka 2013.

130524153502-fast-and-furious-6-vin-diesel-paul-walker-horizontal-large-gallery

Paul enzi za uhai wake akiwa na Vin Diesel katika mojawapo ya filamu za Fast and Furious.

Binti huyo aitwaye Meadow Rain Walker mwenye miaka 16 anailaumu Porsche kwa kifo cha baba yake aliyepoteza maisha baada ya gari alilokuwa akisafiria kugonga taa za barabarani na kuwaka moto Novemba 30, 2013.

Idara ya mahakama ya Marekani imethibitisha kuwa kesi hiyo imesajiliwa.

131130222518-paul-walker-fast-5-horizontal-large-gallery

Paul akiigiza ndani ya Fast and Furious.

Meadow anasema kuwa Porsche haikuzingatia usalama wa madereva na abiria ilipokuwa ikiunda mfumo wa usalama wa magari yake dhidi ya ajali.

Mpaka sasa kampuni hiyo ya Porsche haijajibu mashtaka hayo yanayoikabili.

Uchunguzi wa polisi uliotolewa baada ya miezi minne ulibaini kuwa gari hilo aina ya Porsche Carrera GT,  lililokuwa likiendeshwa na rafiki wa karibu wa marehemu aitwaye Roger Rodas, lilikuwa likiendeshwa kwa kasi.

131130222625-paul-walker-hours-horizontal-large-gallery

Msingi wa kesi hiyo unatokana na ushahidi kuwa gari hilo lilikuwa likienda kwa kasi ya chini lilipopoteza mwelekeo na kugonga taa kwa mujibu wa jarida la TMZ.

Mke wa Rodas mwaka jana aliwasilisha kesi kama hiyo mahakamani ila Porsche ikadai kuwa mumewe ndiye aliyekuwa wa kulaumiwa kwa ajali hiyo wala sio upungufu wa gari lao.

131130230943-paul-walker-2-fast-2-furious-restricted-horizontal-large-gallery

Paul akiwa na Tyrese.

Leave A Reply