Blac Chyna, Rob Wamwagana
NEW YORK, Marekani
PAMOJA na kutarajia kupata mtoto, Blac Chyna na Rob Kardashian wameachana ambapo Rob amefuta picha zote za mpenzi wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ingawa Blac Chyna bado anaonekana kuutaka uhusiano huo.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa habari za mastaa, Rob aliamua kuchukua uamuzi wa kumuacha mpenzi wake huyo baada ya kuona ujumbe mfupi kwenye simu yake ambao haukujulikana ulikuwa ni ujumbe gani kwani mpaka sasa Rob hajaweka hadharani.
Mastaa hawa wamedumu kwenye uhusiano kwa muda wa miezi saba kwani uhusiano wao ulianza Januari mwaka huu. Mwanzo uhusiano wao ulikuwa ukikataliwa na wanafamilia wa Kardashian lakini kutokana na wao kuwapuuzia, waliendelea na mahaba yao hadi leo hii wanapokumbwa na dhoruba