The House of Favourite Newspapers

Black Rhino ‘Kulegeza Vyuma’

Nicholaus Haule ‘Black Rhino’

IKIWA imepita zaidi ya miaka mitatu bila kusikika kwenye gemu, mkali wa michano ambaye pia ni mdogo wa mkongwe wa Bongo Fleva, Prof. Jay, Nicholaus Haule ‘Black Rhino’ amerudi upya kwenye gemu la Hip Hop ambapo leo anatarajia kuachia ngoma yake ya Panda Mnazi ikiwa na maana ya ‘kulegeza vyuma.’

 

Akichonga na Showbiz, Black Rhino ambaye pia anatambulika kama Black Chatta alisema ujio wake huo unamaana kubwa hasa kwa vijana wa sasa kwani unafanya kila anayesikiliza kusahau shida.“Yaani Panda Mnazi ni sawa na kusema kula shangwe, ni ngoma f’lan hivi ya weekend, ya klabu ambayo ikipigwa lazima upagawe.

 

Nimekuja kitofauti kwani ngoma ipo katika mahadhi kama ya ile ngoma ya mistari ambapo kuna mchanganyiko wa Hip Hop na Raga,” alisema Black Rhino. Ngoma ya Mnazi imepikwa na Mr. T Touch huku ‘kioo’ chake kikisimamiwa na Kwetu Studios.

Comments are closed.