Blackberry Kuondolewa Sokoni

Kwa wale watumiaji wa simu za BlackBerry kuanzia sasa kamwe hawataweza kufanya matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe ama kujiunga na intaneti.

Kampuni inayozalisha simu hizo za BlackBerry imesema kuwa itaacha kutumia vifaa vyake vinavyotumia BlackBerry 10, 7.1 OS na matoleo yote ya awali.

 

Hii ikimaanisha kuwa vifaa vyake vya zamani ambavyo havitumiki kwenye programu ya Android havitaweza tena kutumia data, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kuunganisha intaneti ama kupiga simu.

Simu hiyo ambayo ilikuwa maarufu wakati simu janja zilipokuwa zinaanza kutumika kwa wingi miaka ya 2000 haitapatikana tena kuanzia January 4.

 

Mwisho wa matumizi ya simu hizi yanakuja ikiwa ni ndani ya saa 24 tangu kampuni ya Apple kuweka rekodi ya kuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya soko ya dola trilioni 3.Wakati watumiaji wengi wa simu janja wamehama kutoka BlackBerry toleo la mwisho la mfumo wake wa uendeshaji uliozinduliwa mwaka wa 2013 uamuzi wa kusitisha simu zake unatoa tafsiri ya mwisho wa teknolojia kongwe.

 

Kampuni hiyo hapo awali ilitangaza habari hizo mnamo Septemba 2020 kama sehemu ya juhudi zake za kuangazia kutoa programu na huduma za usalama kwa wafanyabiashara, mashirika na serikali kote ulimwenguni chini ya jina BlackBerry Limited.706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment