Blatter, Platini Kortini kwa Ufisadi

 

MAMLAKA za Usalama nhini Uswizi imewafungulia mashtaka maofisa wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter na Michel Platini kwa tuhuma za ufisadi.

 

Katika mashtaka hayo ambapo kesi yao imefunguliwa katika mahakama ya Bellinzona nchini humo, Platin anashtakiwa kwa ulaghai huku Blatter akishtakiwa kwa uhalifu unaohusisha rushwa katika soka.

 

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali nchini Uswizi anasema Blatter, rais wa zamani wa FIFA, alihusika katika mchakato ambao ulikuwa kinyume na sheria kwa kutuma dola milioni 2.19 kwa Platini, ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA).

 

Waendesha mashtaka wamesema kiasi hicho kiliharibu rasilimali za FIFA na kumtajirisha Platin kinyume na sheria skendo ambayo iliihafua FIFA, na kusababisha viongozi hao kuachia ngazi katika nyadhifa zao. Iwapo wakikutwa na hatia dhidi ya mashtaka yanayowakabili, watapewa hukumu ya kifungo cha miaka kadhaa au faini.2177
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment