Bobi Wine Awatoroka Polisi Kwa Bodaboda – Video


MWANAMUZIKI ambaye ni mwanasiasa pia, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere.

Inadaiwa kuwa kwa sasa mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki anaelekea kwenye tamasha lake alilozuiwa kulifanya huko Busabala kwa kutumia bodaboda.

Mapema leo asubuhi polisi walizingira nyumba ya Bobi Wine ili kumzuia kushiriki katika tamasha lake la muziki liitwalo ‘Osobola ku Independence’ kwa Kiingereza ‘Independent Day Music Concert’.

Kwa mujibu wake Bobi Wine, polisi walianza kuzingira nyumba yake na ukumbi wa tamasha hilo jana usiku huku akidai polisi hao ndiyo walisema hawana uwezo wa kulinda watu huko Busabala.

Aidha, Msemaji wa Polisi, Fred Enanga, ameeleza kuwa tamasha hilo haliwezi kufanyika kwa sababu Bobi Wine ameshindwa kutofautisha siasa na muziki.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Loading...

Toa comment