The House of Favourite Newspapers

BOBI WINE YAMKUTA TENA

Related image
Kyagulanyi Robert ‘Bobi Wine’

HUENDA huu ukawa mwaka mbaya kwa mwanamuziki ambaye pia ni Mbunge wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda, Kyagulanyi Robert ‘Bobi Wine’ baada ya kukataliwa kufanya tamasha katika Uwanja wa Mpira wa Mandela nchini humo. Bobi amebaniwa kufanya shoo na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uganda (FUFA). Kupitia mitandao ya kijamii, Bobi amelaumu Serikali yake kwa kumuonea.“Ni kwa vipi wamekuwa wakinizuia? Ni kwa sababu Bobi Wine anahusika! Najua kuwa wanatumia kila mbinu kuzuia biashara zangu na vyanzo vya kupata chochote kitu,” aliandika Bobi Wine na kuongeza:

“Unajua kwa nini? Leo nimepokea barua wamezuia shoo yangu. Sababu? Wanadai eti wamepata oda kutoka FUFA. Hebu angalieni uwanja huohuo unafanya matamasha mengi na hawajawahi kuzuia,” alilalama Bobi.

Miezi michache iliyopita, Bobi na wabunge wengine kadhaa walikamatwa na Polisi wa nchini humo baada ya waandamanaji kupiga mawe gari la Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi. Katika kushikiliwa huko, ilidaiwa Bobi alipitia katika mateso makali.

KAMPALA, Uganda

Comments are closed.