BOCCO ASHANGAZWA NA MABAO YAKE 13 SIMBA

MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John Bocco, amefunguka kuwa anashangazwa na kasi yake ya kutupia mabao ambayo anayo kwa sasa ikiwa ni baada ya kuanza taratibu mwanzoni mwa msimu huu huku muda mwingi akiwa majeruhi.

 

Bocco kwa sasa amefiki­sha mabao 13 katika miche­zo ya ligi, mabao ambayo yanamuweka nafasi ya pili katika chati ya ufungaji bora akizidiwa na mshambuliaji mwen­zake wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye amefunga mabao 18 hadi sasa. Lakini Bocco hakuuanza msimu vizuri kutokana na majeraha na kuwa chini ya kiwango.

 

Bocco aliyetua Simba mwanzoni mwa dirisha la usajili msimu huu ameliambia Championi Ju­matatu, kuwa: “Nimekuwa nikishan­gazwa na mabao yangu ambayo nayafunga kwa sasa. Naamini Mungu ndiye ananijalia kufanya hivi ambavyo nafanya ikiwa ni baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri katika ligi.

 

“Mwanzoni nilisema tageti yangu ni kufunga mabao 10 na kuendelea, nadhani hilo nimeliti­miza kwani nimefanikiwa kuvuka idadi hiyo na utaona nimefunga mabao 13 tena ikiwa ni mfululizo katika kila mchezo wetu jambo ambalo kwangu linanipa matumaini ya kufanya vizuri zaidi.”

Musa Mateja, Dar es Salaam

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment