Bocco Awakata Stimu Yanga

John Bocco

NAHODHA na straika wa Simba, John Bocco ametupa bomu kwa wapinzani wao Yanga kwa kuwaambia watatumia mara mbili ya juhudi walizozionyesha msimu uliopita kuhakikisha wanatetea ubingwa wao kwa msimu ujao. Bocco ambaye yupo kambini na kikosi hicho nchini Afrika Kusini amesema watapambana vilivyo kuhakikisha hakuna timu ambayo itaweza kuwanyang’anya ubingwa wa ligi kuu ambao wanaushikilia.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Bocco amesema kuwa kwa msimu ujao watapambana mara mbili zaidi ya walivyojituma kwa msimu uliopita kuhakikisha wanalibakisha kombe hilo na kulichukua jumla. “Kila kitu ndani ya timu kinaenda sawa na tunaendelea kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu.

 

Katika msimu huo tumejiwekea malengo ya kuhakikisha ubingwa unabaki na tunafika mbali kimataifa. “Yaani kwa msimu huu unaokuja tutatumia juhudi mara mbili ya zile ambazo tulizitoa kwa msimu uliopita, na wamekuja wachezaji wapya basi ninaamini kabisa kwamba tuna nafasi kubwa ya kutetea ubingwa huo,” alisema Bocco.


Loading...

Toa comment