Bocco Awatumia Ujumbe Mzito Yanga
NAHODHA wa Simba, John Bocco, amefunguka kuwa wanakwenda kupata ushindi mnono mbele ya watani zao, Yanga, watakapokutana Mei 8, 2021 Uwanja wa Mkapa.
Bocco alisema anafahamu kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi kwao lakini kwa namna ambavyo wanajiamini na kutaka alama tatu kwenye mchezo huo, haoni nafasi ya Yanga kuchomoka.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Bocco alisema anajua mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa Yanga walianza msimu vizuri na hata sasa, bado wanacheza vizuri lakini wao wana wachezaji bora na watajipanga ili kuhakikisha wanatoka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Mchezo utakuwa mgumu na wala siyo rahisi kama ambavyo watu wanafikiria, Yanga wanacheza vizuri tangu mwanzo wa msimu, lakini sisi tuna wachezaji bora na tutajipanga na kuondoka na alama tatu.
“Niwaombe mashabiki waendelee kutusapoti na waje kwa wingi siku hiyo uwanjani kwani hatutawaangusha,” alisema Bocco.
ISSA LIPONDA,
Dar es Salaam