Bocco: Huyu Luis ni Balaa Lingine

NAHODHA wa Simba, John Bocco, amefunguka uwezo unaoonyeshwa na kiungo mpya wa timu hiyo, Luis Miquissone, raia wa Msumbiji, haupaswi kupuuzwa hata kidogo kwa kuwa unachangia wao kufikia ubingwa wa msimu huu.

 

Bocco ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufikisha pointi 62 baada ya ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara ambao umepigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Bocco alisema kuwa mchezaji huyo kwa sasa ni muhimu kwa Simba kutokana na kuonyesha kiwango bora kadiri siku zinavyokwenda huku akiamini atawasaidia kutetea ubingwa wa msimu huu.

 

“Kiukweli ni mchezaji mzuri, nadhani kila mtu anaona anachokifanya katika kila mchezo, ana kasi nzuri, naamini atazidi kuwa bora zaidi siku zinavyokwenda, ikizingatiwa bado tuna mechi nyingi.

 

“Naamini ni mchezaji mzuri, bado kijana, ana nguvu kubwa, naamini anatusaidia na atatusaidia zaidi kwa siku zijazo pamoja na msimu huu lakini kama ataendelea kuonyesha jitihada zake, namuona akifika mbali katika mchezo wa soka ikiwemo kuhakikisha tunafikia malengo ya msimu huu,” alisema Bocco.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment