The House of Favourite Newspapers

Bocco, Kagere Sasa Vita ni Vita

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck, rasmi sasa anabadilisha mfumo kutoka 4-5-1 na kuwa 4-4-2 akiwatumia washambuliaji wake wawili, Mnyarwanda Meddie Kagere na nahodha John Bocco. Hali hiyo ni wazi sasa itakuwa vita ni vita kwa washambuliaji hao kwenye suala la kufunga. Kagere

ana mabao 12, Bocco mawili. Hiyo ni baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 walipocheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Mbelgiji huyo awali alikuwa akimtumia mshambuliaji mmoja katika michezo iliyopita kati ya Kagere au Bocco huku akijaza viungo wengi kwa ajili ya kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za kufunga.

Sven alisema kuwa anakiri mabadiliko ya mfumo aliyoyafanya ya kuwaanzisha washambuliaji wawili ndiyo yalichangia kwao kupata ushindi mnono walipocheza na Mtibwa. Sven alisema amepanga kuendelea kuutumia mfumo katika michezo ijayo baada ya kuona umempa matokeo mazuri tofauti na awali akiwa anamuanzisha mshambuliaji mmoja. Aliongeza kuwa kitendo cha kuwaanzisha

pamoja Kagere na Bocco kiliwachanganya wapinzani wao Mtibwa kutokana na kutotambua haraka mchezaji gani wa kumdhibiti. “Hakuna kingine kilichotupa ushindi katika mchezo wetu na Mtibwa zaidi ya kujituma kwa wachezaji wangu, hiyo ndiyo siri kubwa ya ushindi katika mchezo huo ambao ulikuwa mgumu. “Kingine ni uamuzi wangu wa kuwaanzisha kwa pamoja Bocco na

Kagere ambao umechangia kuwavuruga wapinzani wangu kutokana na wote kuwa tishio kwa mabeki. “Nimefurahishwa na jinsi ambavyo vijana wangu walivyopambana wakishambulia kwa kasi kwenye goli la wapinzani wetu, hivyo ndivyo ninavyotaka kuona wachezaji wangu wakicheza katika michezo ijayo na utakuwa ndiyo mfumo wetu,” alisema Sven.

WILBERT MOLANDI,   Dar es Salaam

YANGA HII SI MCHEZO! MAZOEZI Tu HATARI, Hao TZ PRISON Wajiandae..

Leave A Reply