Bocco: Tunaanza Na Ubin Gwa Wamapinduzi

NAHODHA na mshambuliaji wa Simba, John Bocco ametamba kwamba watauanza mwaka huu mpya kwa kulichukua Kombe la Mapinduzi ambapo litakuwa kombe lao kwa kwanza kwa msimu huu.

 

Bocco ataiongoza Simba katika michuano ya Mapinduzi Cup ambayo ilianza kurindima jana Jumanne visiwani Zanzibar. Simba wamepangwa kundi A na timu za Chipukizi, Mlandege na KMKM.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Bocco amesema kwamba wanalichukulia kwa umakini mkubwa kombe hilo ambapo lengo ni kulitwaa.

 

“Tunaenda huko Zanzibar tukiwa na lengo la kutaka kutwaa ubingwa huo wa Mapinduzi na tutachukulia siriazi kila mechi ambayo tutashuka dimbani.

 

“Tunataka hili liwe kombe letu la kwanza kwa msimu huu na ninajua tutalifanikisha hilo kwa sababu ya maandalizi tuliyoyafanya,” alisema Bocco.

Simba wanaondoka leo Jumatano kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki kombe hilo.

STORI NA SAID ALLY | CHAMPIONI

Loading...

Toa comment