Bocco: Tunawafunga Yanga Fainali Shirikisho

MSHAMBULIAJI na nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco ameweka wazi kuwa, kikosi chao kimejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili ijayo.


Simba na Yanga zitakutana Jumapili ijayo
ya Julai 25, katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho utakaochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara wataingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga Julai 3, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.Bocco amekuwa katika kiwango bora msimu huu, ambapo amefanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 16.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Bocco alisema: “Tunatarajia kukutana na mchezo mgumu wa fainali dhidi ya Yanga, hii ni kwa sababu wapinzani wetu wana timu nzuri na tunawaheshimu kwa hilo.

 

“Lakini nasi tuna timu nzuri sana, hivyo tunakwenda kufanya maandalizi yaliyokuwa bora na tunaamini katika maandalizi yetu kuwa tunakwenda kushinda mchezo huo.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam3403
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment