The House of Favourite Newspapers

Bodaboda Mtandao Sasa Waula Kwa Dili Jipya la Kubeba Vifurushi

0
Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania akizungumza kwenye uzinduzi huo kulia ni Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Munira Ruhwanya.

Dar es Salaam, 30th August 2024:Waendesha bodaboda wanaofanyakazi na kampuni ya huduma za usafiri mtandaoni Bolt wamepata dili jipya baada ya leo kampuni hiyo kuzindua huduma mpya ya usafirishaji wa vifurushi ijulikanayo kama ‘Bolt Send’ katika jitihada za kampuni hiyo za kupanua wigo wa huduma zake kwa wateja.

Huduma ya Bolt Send imezinduliwa ili pia kuweza kutumia fursa ya  kukua kwa huduma za usafirishaji wa vifurushi ambazo zinakua nchini Tanzania.

Baadhi ya waendesha bodaboda wakielezea jinsi huduma hiyo mpya itakavyowaongezea kipato.

Kwa sasa huduma hii inapatikana jijini Dar es Salaam pekee na inawezesha wateja kupata huduma za haraka, kuaminika na zenye gharama nafuu na hivyo kutilia mkazo sifa ya Bolt ya kuwa mwanzilishi wa huduma zinazomlenga mteja.

Ikiwa imebuniwa kwa matumizi rafiki ambayo yameunganishwa kwenye programu timizi (applikesheni) ya sasa ya huduma za usafiri wa mtandaoni, wateja wanaweza kutuma vifurushi vyenye ukubwa tofauti kwa eneo lolote ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Huduma hii imesanifiwa ili kukidhi mahitaji mapana ya usafirishaji wa vifurushi, kuanzia nyaraka muhimu na za haraka za kiofisi mpaka bidhaa binafsi huku usafirishaji ukizingatia uangalizi maalum na weledi.

Uzinduzi wa huduma mpya ya Bolt Send utaleta mabadiliko makubwa si tu kwa mteja mmoja mmoja bali pia kwa wajasiriamali wakati na wadogo.

Wafanyabiashara wakiwa na uwezo wa kutuma na kupokea vifurushi kwa ufanisi wataweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao, kupanua wigo wa masoko na kurahisisha undeshaji wa biashara zao.

Bolt Send inatarajiwa kuchochea kukua kwa biashara za wazawa kwa kuwapatia nyenzo muhimu wanazohitaji katika soko lenye ushindani.

Meneja Mkuu wa Bolt, Dimmy Kanyankole, alisema; “Uzinduzi wa huduma yetu ya usafirishaji wa vifurushi inaashiria hatua muhimu katika dhima yetu ya kurahisisha na kuimarisha maisha ya kila siku ya wateja wetu.

“Tunajivunia kutoa huduma inayochanganya kasi, uhakika na unafuu wa bei, na inayohudumia mahitaji mbalimbali ya Watanzania. Huduma hii mpya inaakisi dhamira yetu ya kuchochea ubunifu na kuchangia ukuaji wa biashara za wazawa nchini.

Huku ikichagizwa na umuhimu wa usalama na uwazi katika usafirishaji, Bolt Send inajumuisha kifaa maalumu cha kisasa cha kufuatilia mwendo, ambapo mteja ataweza kufuatilia usafirishaji wa mzigo wake kuanzia kinapochukuliwa mpaka kinapofikishwa kwa anayepokea.

Leave A Reply